Mkuki Na Nyota Publishers

Faradhi Ya Moyo

Sh 18,000

Anna Samuel Manyanza

SKU: 9789987084456 Categories: , , Tag:

Ugumba unaweza kuwa sumu kwenye ndoa. Wasila yamemkuta. Kapewa talaka na mumewe, Maulidi, kwa vile hatungi mimba. Maulidi akaoa upya, tena zaidi ya mara mbili. Hakuna katika hawa wakeze aliyeweza kutunga mimba. Huba la Maulidi kwa Wasila likachipua upya. Akamtaka Wasila arudi kwa udi na uvumba, kwa mikuki na mapanga.

Lakini Wasila alishapelekwa Unguja kwa shangaziye na mjombawe ili walimwengu wasimuandame kwa macho yao ya paka na ndimi zao za swila. Unguja ikamkutanisha Wasila na Bilali.Ugumba wa Wasila ukachukua taswira nyingine. Tumbo la Wasila likaanza kutuna. Ni mimba au ni uchuro? Wasila a Bilali wakajikuta wanaelea kwenye bahari ya matumaini ila yenye wimbi la kuzamisha. Bahari ya matumaini ikachafuka. Wimbi likazamisha matumaini ya Wasila na Bilali. Moyo wa Bilali ukachukua taswira pacha. Taswira pacha? Yanawezekanaje mambo haya?

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Faradhi Ya Moyo”

Your email address will not be published. Required fields are marked *