Mkuki Na Nyota Publishers

Mzoga Unaonukia

Author(s): binadamu, diwani, Kampala, Kiswahili, Lenard Mtesigwa, mtu, Safal-Cornell, ushairi

Sh 12,000

Diwani ya ushairi ya Kiswahili ya Lenard Mtesigwa, mwandishi wa orodha fupi ya Safal-Cornell. Ubini wa kichwa ni dhana ya binadamu (mzoga) na mtu (kunukia) kama viumbe viwili vyenye nasaba moja: maovu na mema vikishindana ndani ya kiumbe kimoja.

ISBN: 9789987753109 Category: Tags: , , , , , , ,

Diwani ya ushairi ya Kiswahili iliyoandikwa na Lenard Mtesigwa, mwandishi aliyekuwa kwenye orodha fupi ya Tuzo ya Safal-Cornell. Diwani hii imeibua dhana moja kuu ambayo pia ni mhimili wa jina la kitabu: binadamu na mtu. Mbali na ukweli kuwa mtu na binadamu ni majina mawili tofauti yanayorejelea kiumbe kimoja, katika diwani hii yanaonekana ni viumbe viwili tofauti ila vyenye nasaba moja: binadamu akiwa amebeba dhana ya mzoga, na mtu mumo humo, utu ukiwa amebeba dhana ya kunukia. Kwa maana nyingine, binadamu ni yule kiumbe razini mwenye chembechembe za uhayawani ndani yake, ilhali mtu ni kiumbe razini aliye katika ukamilifu wa urazini kwa matendo pendekea katika jamii ya warazini. Dhana inaibua maovu (mzoga) na mema (kunukia). Lenard Mtesigwa ni mwandishi wa tamthilia, riwaya, na hadithi fupi za Kiswahili, aliyeanza kazi ya utunzi mwaka 2015 katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala cha Tanzania.

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Mzoga Unaonukia”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…