Mkuki Na Nyota Publishers

Bweni la Wasichana

Sh 15,000

Lucas Lubago

Usiku huo nilikuwa nasimamia maandalizi ya masomo ya usiku. Nikapigiwa simu na Rose, nikaipokea. Wakati naongea naye, nikawa natembea taratibu kama naelekea kwenye mabweni. Ghafla, nikaona taa za bweni wanalolala “Buibui” zinawaka na kuzima, nikajua ni hitilafu katika mfumo wa umeme. Nikataka kusogea ili nithibitishe kisha nitoe taarifa mapema kwa uongozi na matengenezo yafanyike.

Nilisogea mpaka mlangoni, taa zikawaka moja kwa moja, na kwa kuwa kulikuwa na dalili za kuwemo mwanafunzi, nilitaka kujua kwanini hayupo darasani wakati wenzake wote walikuwa wana jisomea. Niliingia nikakuta hali ya ukimya sana, nikatembea mpaka karibu na mwisho wa bweni, nilichokiona ni aibu kubwa! Huwezi amini, “Buibui” waliponiona wakadondosha khanga! Huwezi amini, “Buibui” waliponiona wakadondosha khanga! Wakabaki kama walivyozaliwa…

Kuhusu Mwandishi

Lucas Gervas Lubango ni mwalimu wa masomo ya biashara (Accountancy & Commerce). Alisoma Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Kibaha (ECA). Elimu ya juu aliipata katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, akisomea Ualimu katika Masomo ya Biashara (Degree of Education in Commerce).

Bweni la Wasichana ni riwaya yake ya kwanza kuandika na imeshika nafasi ya pili kwenye Tuzo ya Safal Cornell ya mwaka 2021.

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Bweni la Wasichana”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…