Hii ni riwaya ya kwanza ya Mbwana Kidato ambayo inatokana na tukio la kweli alilolisoma alipokua akipitia majarida mbali mbali ya Tanzania kwenye mtandao. Kwenye kurasa za mbele, alikutana na Habari ya kuhuzunisha. Ilikua ni Habari ya msichana mwenye ulemavu wa Ngozi aliyekatwa viungo vya mwili wake.
Hii ni kazi ya mwandishi, kazi ya kufikirika, yenye kuelimisha, kuakaisi Maisha yetu na kutuuliza msawali juu ya utu wetu. Je miongoni mwetu kuna wengine wana utu wenye thamani zaidi ya utu wa wengine? Kama kuna kipimo cha utu, huo utu unapimwa na kipimo cha aina gani? Je kipimo hicho ni maumbile yetu au ni tabia zetu? Ama ni vitu vinavyo tuzunguka? Muandishi anajaribu kuuliza haya maswali, kupitia mhusika mkuu wa riwaya hii ambaye ni ‘SINAUBI‘
Kuhusu Mwandishi
Mbwana Kidato ni mtengenezaji wa vipindi vya runinga na filamu. Amepata elimu yake nchini Uingereza kwenye Nyanja za uandaaji, utengenezaji, uandishi na uhariri wa picha za vipindi vya filamu na runinga. Ameshawahi kufanya kazi na shirika la Utangazaji la Tanzania, kama mtayarishaji wa vipindi.
Siyo mara yake ya kwanza kuandika, (film scripts) lakini kazi yake imekuwa ikilenga zaidi hadhara ya upande wa runinga. Safari hii ameandika riwaya/tamthilia kwa hadhara yote, yaani hadhara ya wasomaji vitabu na hadhara ya waangaliaji runinga na filamu.
Reviews
There are no reviews yet.