Mstahamilivu hula mbivu, mtaka cha uvunguni sharti ainame, na mchumia juani hulia kivulini. Ni machache ya maadili yamuongozayo binti Malaika katika safari yake ya kutimiza ndoto zake. Kujiendeleza kielimu ndiyo ndoto yake kuu. Kwa vile Mungu hamtupi mja wake, anabahatika kwenda ughaibuni kitaaluma. Ni safari inayomtenganisha na mpenzi wake, Ben. Lakini Ben anaahidi kumsubiri hadi afuzu masomo yake. Katika kipindi hiki cha utengano, dunia inawapangia mambo mengine kabisa, ni utengano unaotishia kulisumu penzi lao. Majaribu hayeshi, vishawishi ni vingi. Penzi lao linayumba, linatishia kudumbukia kwenye dimbwi la damu. Lakini Malaika haliachii penzi lake kwa Ben, analipigania kishujaa. Ben pia anaingia vitani kulipigania penzi la Malaika. Je, watashinda vita hivi vya kimapenzi?
Kuhusu Mwandishi
Anna Samwel Manyanza ni mwanafasihi wa riwaya na hekaya za watoto. Riwaya yake hii ya kwanza, ilishinda Tuzo ya Kiswahili ya Mabati – Cornell ya Fasihi ya Afrika.
Riwaya yake mpya inaitwa Faradhi ya Moyo
Reviews
There are no reviews yet.