Hiki ni kitabu cha Tano na cha mwisho katika mfululizo wa vitabu vya Uwazi na Ukweli. Mfululizo huu wenye hotuba za kila mwisho wa mwezi
za Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin W. Mkapa, una malengo makuu matatu:Kwanza ni kufanya hotuba hizo kuwa chanzo kimojawapo cha elimu ya
ziada, hasa kuhusu mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa, sababu zake na mwelekeo wa mambo hayo.
Pili, hotuba hizo zilikuwa sehemu mojawapo ya uwajibikaji wa Rais kwa Wananchi, kwani alikuwa na wajibu wa kuwajulisha yale aliyokuwa akifanya na sababu zake.
Tatu, hotuba hizo ni mwendelezo wa juhudi za awamu zote za uongozi wa nchi yetu kuimarisha misingi ya utawala bora.
Reviews
There are no reviews yet.