Riwaya ya Kiswahili iliyoandikwa na C.G. Mung’ong’o. Gusto, kijana mdogo wa shule, hakurithi mali ya marehemu baba yake tu, bali pia amerithi tunguri zake, madaraka yake ya kiwanga, na mlolongo mzima wa visa, visasi, na vinyongo vya baba yake. Urithi huu unamtoa Gusto katika ulimwengu wa wachawi. Hatimaye, baada ya kupambana na vitimbi, hasara, na mikasa ya kutisha, inambidi Gusto akate shauri kati ya kuyatekeleza matakwa ya marehemu baba yake na kuyatimiza matakwa ya dhamiri yake binafsi na ya jumuiya yake inayotafuta maendeleo ya kisasa. Mvutano unaotokea unakiuka uwezo wake alioupata shuleni na kutisha kumrarua vipande vipande. Hiki ni kisa cha kutisha na kutaharakisha, kinachotuingiza katika undani wa uganga wa uchawi na mazingaombwe, na hatimaye kutuacha tukijiuliza kama kweli mambo hayo yanayo manufaa yoyote kwa jamii yetu au ni doa na mirathi ya hatari tu katika utamaduni wetu.

Mirathi ya Hatari
Author(s): C.G. Mung'ong'o, Kiswahili, mazingaombwe, riwaya, Tanzania, uchawi, urithi, utamaduni
Sh 8,000
Riwaya ya Kiswahili ya C.G. Mung’ong’o. Gusto anarithi tunguri na madaraka ya kiwanga ya baba yake, na lazima achague kati ya matakwa ya marehemu na matakwa ya jamii yake inayotafuta maendeleo. Riwaya ya kutisha inayochunguza mpasuko kati ya desturi za kale za uchawi na mtazamo wa kisasa.
| Weight | 0.2 kg |
|---|---|
| Binding |




Reviews
There are no reviews yet.