Mkuki Na Nyota Publishers

Uwazi na Ukweli – 4

Sh 7,000

B. W. Mkapa

Hiki ni kitabu cha Nne katika mfululizo wa vitabu vya Uwazi na Ukweli vyenye mkusanyo wa hotuba za kila mwisho wa mwezi za Mheshimiwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Benjamin W. Mkapa.

Katika Toleo hili Rais anajadili kwa uwazi na ukweli juu ya masuala mbalii mbali ya muhimu kwa taifa, kama vile:

Ulazima wa kuweka Bajeti Ndogo ili kugharimia athari za ukame kama vile uhaba wa chakula na ugharimikiaji uzalishaji wa umeme; pia gharama za uandaaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura;
Ripoti ya Tume ya Kimataifa kuhusu Masuala ya kijamii katika Utandawazi na umuhimu wa kufanya juhudi za kuepuka athari za utandawazi kuanzia nyumbani;
Ushirikiano wa utatu kati ya Serikali, wananchi na wahisani katika kupiga vita umaskini;
Umuhimu wa kushiriki katika Tume ya Kimataifa iliyoanzishwa na Mheshimiwa Tony Blair, Waziri Mkuu wa Uingereza;
Dhana halisi ya Bajeti ya Taifa na namna dhana hiyo inavyotakiwa kueleweka; na
Dhima ya wananchi na Serikali katika vita dhidi ya ugonjwa waPia mheshimiwa Rais anazungumzia umuhimu wa wananchi katika kushiriki- ana na jeshi la polisi ili kupunguza wimbi la uhalifu. Anaeleza pia uanzishaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) kufuatia mafanikio makubwa ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya msingi (MMEM) hatimaye anaeleza kuhusu Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA), hali ya siasa nchini na uhusiano na ushirikiano na mataifa ya nje.

Dimensions 205 × 143 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Uwazi na Ukweli – 4”

Your email address will not be published. Required fields are marked *