Mkuki Na Nyota Publishers

Uwazi na Ukweli – 2

Sh 7,000

B. W. Mkapa

Katika kitabu hiki cha pili kwenye mfululizo wa vitabu
vinavyokusanya hotuba zake za kila mwisho wa mwezi (cha tatu
kinaandaliwa), Rais Benjamin W. Mkapa anazungumzia matukio
mema na mabaya ya mwaka 2002, pamoja na hatua za maendeleo
zilizopigwa na taifa katika nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Rais Mkapa anaeleza kwa kina maana na athari za utandawazi
kwetu kama taifa na kwa watu binafsi. Aidha anaendelea kueleza,
kufafanua na kutetea sera ya ubinafsishaji na kuonyesha matunda
ya sera hiyo bila kupuuza sokomoko kama ile iliyofuatia hatua
ya kubinafsisha shirika la TANESCO.

Rais Mkapa anaelezea vilevile masuala ya siasa, hasa utekelezaji
mzuri wa MWAFAKA kati ya CCM na CUF kule Zanzibar
ulioashiria utulivu wa kisiasa nchini na kurejesha upendo na
mshikamano wa wananchi Visiwani.

Kwa wale wote wanaopenda kufuatilia historia ya taifa letu,
hotuba hizi za Rais Benjamini W. Mkapa ni kumbukumbu nzuri
na ya kudumu ya miaka ya uongozi wake. Ni muhimu pia kwa
viongozi, walimu na wanafunzi wa ngazi zote katika kuelewa na
kuelezea masuala ya siasa, jamii na uchumi wa Tanzania.

Dimensions 203 × 127 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Uwazi na Ukweli – 2”

Your email address will not be published. Required fields are marked *