“Tangu mwanzo kabisa wa Serikali ya Awamu ya Tatu nilisema kuwa
sera yangu ni Uwazi na Ukweli. Na niliwaambia viongozi wenzangu,
kwenye Chama Cha Mapinduzi na kwenye Serikali, kuwa ni afadhali
nichukiwe kwa kuwa mkweli, kuliko kupendwa kwa kuwa mwongo na
mlaghai. Nilipotamka hivyo, wapo waliosema huo ni ushahidi kuwa
mimi si mwanasiasa. Lakini nafurahi kuwa wananchi walinielewa, na
wakaniamini.
“Hotuba zangu za kila mwisho wa mwezi kwao ni mojawapo ya jitihada
zangu za kuhakikisha wanajua Serikali inafanya nini, kwa sababu gani,
na kwa faida gani kwao. Si haki kuwaongoza wananchi kwenda
wasikokujua, au bila kuwaeleza sababu za kwenda huko. Serikali
inayojiamini, na inayowajibika kwa wananchi, inakuwa wazi kwao.
Haina sababu ya kujificha. Kiongozi aliyejiridhisha kuwa jambo fulani
ni la manufaa kwa wananchi wake hana sababu za kuogopa kuwa
mkweli, na kuelezea kwa nguvu ya hoja, kwa nini sera, mikakati na
mambo fulani ni ya lazima. Ni vema, na haki, kuongoza walioelewa,
kuliko kuongoza walioachwa gizani.”
Hivyo ndivyo asemavyo, Mheshimiwa Rais Benjamin W. Mkapa katika
utangulizi wa kitabu hiki cha kwanza katika mfululizo wa vitabu vya
hotuba zake za kila mwisho wa mwezi kwa wananchi.
Hotuba hizo ni ufunguo wa uelewa sahihi wa siasa, uchumi na masuala
ya jamii katika nchi yetu katika kipindi hiki cha historia. Umoja wa
taifa, mshikamano na juhudi za maendeleo yanahitaji kipaumbele
maalum katika dunia ya leo ya utandawazi, na Mheshimiwa Rais
Mkapa anaeleza kwa ufasaha ni nini tunapaswa kufanya ili tuweze
kufanikiwa.
Uwazi na Ukweli – 1
Sh 7,000
Weight | 0.4 kg |
---|---|
Dimensions | 207 × 145 mm |
Binding |
Reviews
There are no reviews yet.