Mkuki Na Nyota Publishers

Ujanajike

Author(s): Dotto Rangimoto, Kabula, Kiswahili, mfumodume, Morogoro, riwaya, Safal-Cornell 2022, ujanajike

Sh 15,000

Riwaya ya Kiswahili ya Dotto Rangimoto, mshindi wa Tuzo ya Safal-Cornell 2022 (ushindi wake wa pili, baada ya Mwanangu Rudi Nyumbani 2017; mtu wa kwanza kushinda mara mbili katika vipengele tofauti). Kabula anakabiliwa na mfumodume; mjukuu wake anaapa kupambana. Related: Row 173.

Riwaya ya Kiswahili iliyoandikwa na Dotto Rangimoto, mshindi wa Tuzo ya Kiswahili ya Safal-Cornell ya Fasihi ya Afrika mwaka 2022. Huu ni ushindi wake wa pili wa tuzo hiyo, baada ya kushinda mwaka 2017 na diwani yake Mwanangu Rudi Nyumbani (Row 173), ikimfanya kuwa mtu wa kwanza na wa pekee kushinda Safal-Cornell mara mbili kwenye vipengele tofauti. Kabula anazaliwa na kulelewa katika jamii inayotawaliwa na mfumodume. Anasimanzika kufukuzwa shule kwa sababu ya ujauzito huku aliyeshiriki naye ngono akiendelea na masomo hadi chuo kikuu. Wakati Kabula akiwa fukara mwenye jukumu la ulezi, mwenzake anakuwa Rais wa nchi asiyejali mtoto wake wa ujana. Katika hali isiyotarajiwa, Kabula anashuhudia mjukuu wake akifukuzwa shule kwa sababu ileile iliyomsibu yeye. Kabula alikubali kuishi chini ya mfumodume, lakini kwa mjukuu wake mambo ni tofauti kabisa: ameapa kupambana na mfumo huo.

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Ujanajike”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…