Mkuki Na Nyota Publishers

Tawasifu ya Balozi Daniel Ole Njoolay

Authors: Daniel Ole Njoolay

Sh 35,000

ISBN: 978-9987-08-574-3 Categories: , , , , Tag:

Balozi Daniel Ole Njoolay ni nani hasa?
Kutoka kijiji cha Olkokola chini ya Mlima Meru, alikua kijana kutoka umasaini aliyepata nafasi ya kusoma kwa miujiza. Akivushwa na changamoto mara nyingi kwa kushikwa na mkono wa tatu, kama yeye mwenyewe anavyoeleza, safari yake ikamfikisha kwenye nafasi ambazo hakuwahi kuzi-tarajia: kiongozi mkoani, balozi nchi za nje, na mwakilishi wa Tanzania katika majukwaa ya kimataifa.

Lakini hii si hadithi ya cheo na madaraka pekee. Ni simulizi ya mtu aliyeamini hakuna kisichowezekana; mtu aliyeinuliwa na mkono usioonekana, na ambaye kila hatua ya maisha yake imekuwa ushuhuda wa imani, nidhamu, na ujasiri.

Tawasifu ya Balozi Daniel Ole Njoolay ni kioo cha historia ya Tanzania kupitia macho ya mmoja wa watumishi wake waaminifu. Hii ni simulizi ya kushangaza, ya kutia moyo, na yenye mvuto na hamasa kubwa kwa watu wa rika zote lakini haswa kwa vijana wa kizazi hiki na vijavyo.

“Sifa zake ni mfano wa kuigwa. Amefanya kazi ndani ya umma kwa bidii, ubunifu, uadilifu na uaminifu. Amekuwa mshauri mzuri na anashauri anachoamini siyo kwa kupendeza. Nimekisoma kitabu hiki kwa msisimko na kina mengi ya kujifunza, hasa vijana wanaoanza maisha ya utumishi na uongozi.”– Joseph Sinde Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

“Mkuu! Ninachokupendea huwa unasema ukweli hata kama ule ukweli unaniumiza…” – Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Tawasifu ya Balozi Daniel Ole Njoolay”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…