Mkuki Na Nyota Publishers

Safari Ya Matumaini

Author(s): John Wanyonyi, Kenya, Kiswahili, Mfanisi, Moi's Bridge, riwaya, Safal-Cornell, Tanzania

Sh 18,000

Riwaya ya Kiswahili ya John Wanyonyi, mshindi wa Tuzo ya Safal-Cornell. Mfanisi, mtoto wa mama pekee, anajisaka kuanzia chekechea kupitia Moi’s Bridge, Mwanza, Nakuru, na Mombasa. Maudhui mseto: ndoa, mahusiano ya vyote vizazi, talanta, elimu, usaliti, siasa, uongozi.

Riwaya ya Kiswahili iliyoandikwa na John Wanyonyi, mshindi wa Tuzo ya Safal-Cornell. Mfanisi anaanza safari yake ya kujisaka punde akiwa shuleni katika madarasa ya malezi na chekechea. Anatembea katika dunia anayojiona akiwa pekee katika ulimwengu wa familia za wazazi wote wawili, kinyume naye aliye na mama pekee. Dunia yake inampelekea kuwa na marafiki tofautitofauti kuanzia Moi’s Bridge huko Kenya, Mwanza Tanzania, na mara tena Nakuru na Mombasa nchini Kenya. Maisha yake yanaathiriwa pakubwa na ama marafiki zake au familia yake. Katika riwaya hii, msomaji atakumbana na maudhui mseto yanayoathiri kizazi cha leo na kijacho: maisha katika ndoa, mahusiano ya vijana kwa vijana, mahusiano ya wazee kwa vijana na wazee kwa wazee, talanta, elimu, bidii na kazi, usaliti maishani, unafiki, siasa, na uongozi. Ni kazi inayomulika maisha ya leo na jinsi masuala ibuka yanavyoathiri jamii kwa namna hasi au chanya.

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Safari Ya Matumaini”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…