Mpelelezi mashuhuri wa Afrika, Mtanzania, Willy Gamba, akiwa likizoni huko Afrika Magharibi, jijini Freetown, Sierra Leone, anatumiwa ujumbe wa haraka arudi upesi nchini kwani kumetokea hujuma kubwa.
Kutokana na uzalendo wake hapotezi muda, hima anarejea nchini. Chifu wake anamweleza kuwa shehena kubwa ya silaha za kivita ambazo ni mali ya wapigania uhuru wa kusini mwa Afrika, imeibiwa bandarini, katika mazingira ya kutatanisha.
Habari hizi zinaleta utata mwingi, baadhi ya nchi zikisema ni njama za Makaburu, na nyingine zikisema ni njama za Tanzania.
Katika kiza kinene kinachozunguka suala hili, serikali ya Tanzania inamtuma Willy kuwasaka. Hapo ndipo patashika zinaanza na jiji la Dar es Salaam linakumbwa katika wimbi la msukosuko wa uhaini, usaliti, na mauaji ya kikatili…
Fakih Mzee –
napenda story za hyu mwamba