Mkuki Na Nyota Publishers

Methali, Semi na Vitendawili vya Kisambaa

Sh 10,000

Yussuf Rajabu Makamba

“Mimi ni Msambaa, lakini sikuzaliwa Sambaani na sikukulia huko. Nakijua kisambaa lakini sizijui methali, semi na vitendawili vya kisambaa. Mtindo wa Mzee Makamba wa kutoa hutuba na kunukuu methali za kisambaa, unanivutia sana. Kutokana na umalenga wake wa kuzijua kwa ufasaha methali za kisambaa, nimemshauri azikusanye methali hizo na kuziandika katika kitabu ili asije akafa nazo. Namshukuru amekubali kutuachi urithi huo, ameandika kitabu hiki amba- cho tunacho mkononi. Nawaomba sasa vijana waliozaliwa na kukulia katika mazingira kama yangu, tukisome kitabu hiki. Hiyo ndio namna nzuri ya kumshukuru Mzee Makamba. Tujuacho kitone.”

–January Y. Makamba, Mbunge wa Bumbuli

Kuhusu Mwandishi:

Mwandishi wa kitabu hiki, Yussuf Rajabu Makamba, ni mkulima na mfugaji. Amewahi kuwa Mbunge, Katibu Mkuu wa CCM, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, na ni Afisa Mstaafu wa JWTZ. Amewahi pia kuwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kigoma na Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa.

Mwandishi ameandika vitabu vingi ikiwemo ‘Cha Kale ni Dhahabu’.

Weight 0.4 kg

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Methali, Semi na Vitendawili vya Kisambaa”

Your email address will not be published. Required fields are marked *