Watu wa mauzo waliopata mafanikio hawafanyi vitu tofauti; wanafanya vitu kwa namna tofauti.
Umewahi kujiuliza ni kwa nini baadhi ya biashara au watu wa mauzo huweza kujizolea wateja wapya mwezi hata mwezi huku wakiendelea kuwa na wateja wao wa zamani? Na papo hapo wengine wanafunga biashara kwa kushindwa kupata wateja wa kutosha?
Mafanikio yako yatatokana na mambo yafuatayo:
Uwezo wako wa kupata wateja wapya na kubakiza wale wa zamani.
Kutengeneza mazingira yatakayomfanya mteja arudi tena na tena kununua bidhaa au huduma.
Kutumia wateja walioridhishwa na huduma zako kukutangaza.
Kuwafanya wateja wenye hasira na malalamiko kupata furaha na kuridhika.
Mbinu za Kuwapata Wateja na Kubaki Nao, kinakufundisha jinsi ya kufanikiwa katika eneo moja litakalokuonesha endapo biashara yako inainuka au inaanguka.
Murori Kiunga ni mjasiriamali, mkufunzi na mwandishi mahiri kutoka Nairobi, Kenya. Vitabu vyake maarufu vinajumuisha:
The Art of Entrepreneurship (hii ni tafsiri yake ya kiswahili)
The Winning Character: Succeeding Where Others Fail, The 7 Pillars of Financial Success, The Entrepreneurial Journey.
From Employmemnt to Business and Common Reasons why start-up Business Fail and what you can do about it.
Reviews
There are no reviews yet.