Mkuki Na Nyota Publishers

Kanga ya Mama

Author(s): Maria G. N. Biswalo, Theresia Mmasi

Sh 25,000

ISBN: 9789987085910 Categories: , , Tags: ,

Kanga ni nguo ya jadi inayovaliwa na baadhi ya wanawake wa Afrika Mashariki.

Je, umewahi kujiuliza ni njia ngapi zipo za kutumia kanga? Usijiulize zaidi! Tumbukia kwenye hadithi hii inayosimuliwa na mtoto juu ya kanga ya Mamaye, na jinsi kanga hiyo inavyofungua wezekano zisizo na mwisho ujipatie majibu!

Maria G. N. Biswalo | Mwandishi

Kama mwalimu wa kimataifa na mama wa watoto wa tamaduni mbili, Maria G. N. Biswalo alibaini ukosefu wa uwakilishi katika maandishi ya hadithi za watoto wadogo, zionyeshazo tamaduni yake ya Kitanzania na lugha mama- Kiswahili. Kupitia hadithi zake, Maria ana matamanio ya kuziba pengo hili kwa kuibua na kuhamasisha upatikanaji rahisi wa hadithi nyingi za watoto za Kitanzania duniani kote. Anakualika kuungana naye kupitia tovuti ya www.hadithizamama.com.

Theresia Mmasi | Usanifu wa Picha

Theresia Mmasi ni mtengenezaji wa taaluma anuwai wa Kitanzania na anayependa michoro, historia na elimu ya sanaa. Yeye si tu ana fikra bunifu, bali pia muundaji na mtendaji. Theresia anajishughulisha na miradi inayotumia sanaa ya picha kama zana ya kuunda ulimwengu jumuishi zaidi, endelevu, na wa haki. Anaaminikuwa ufundi wa picha ni zana wazi inayowezesha jamii zenye changamoto kumiliki na kusimulia hadithi zao.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Kanga ya Mama”

Your email address will not be published. Required fields are marked *