Kamusi yoyote ni kazi ya maarifa, ni chemchemi ambayo maji yake hayakauki, hutiririsha maarifa na kuchochea watumiaji kutaka kuijua zaidi. Kamusi ya Ukristo inazo sifa hizi, na za ziada kwani ni kamusi ya kwanza kwa lugha ya Kiswahili ambayo inaweka pamoja tafsiri ya dhana mbalimbali, majina mbalimbali ya Wakristo na desturi za Makanisa ya Kikristo.
Kamusi ya Ukristo ni kamusi ambayo kwa umahiri mkubwa mwandishi amefuatilia na kufanikiwa kukusanya vitomeo vinavyowakilisha madhehebu mbalimbali ya Kikristo. Kuna vidahizo ambavyo hutumiwa zaidi na dhehebu moja kuliko lingine, lakini mwandishi ameviweka pamoja ili kuuondoa umadhehebu na kuujenga umoja wa Ukristo. Ni ukweli usiopingika kuwa waamini wengi hawaelewi misamiati na istilahi nyingi za dini zao. Hivyo basi kwa msaada wa Kamusi hii, msomaji atafaidi maarifa ya maana na matumizi ya maneno si tu ya dhehebu lake, bali Ukristo kwa ujumla wake.
Reviews
There are no reviews yet.