Akiwa hana kitu zaidi ya kalamu yake, mwandishi wa habari, Walari Saire, anaamua kupambana na mfumo kandamizi, uliojaa rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa rasilimali za nchi, hatua inayomweka katika hatari kubwa ya kupoteza maisha yake yeye na familia yake. Hatimaye alifungwa kwa kubambikwa kesi. Pamoja na madhila anayopitia huku watu wake wa karibu wakimwonya na kumtaka aache kufuatilia ‘mambo ya wakubwa’, Walari anaamua kutorudi nyuma lakini makubwa yanampata. Anaanza kupoteza watu wake wa karibu sana. Ni yeye sasa, aamue kusuka ama kunyoa.
Fuatana na mwandishi mahiri, Walari Saire katika mkasa huu wa Gereza la Kifo.
Kuhusu Mwandishi
Hamisi Hussein Kibari ni mtunzi wa riwaya na mashairi. Pia, ni mwandishi wa habari, mhariri na mtengeneza filamu. Kwa kipindi cha takribani miaka 20, Hamisi ameandika hadithi katika magazeti mbalimbali nchini Tanzania na baadhi ya hadithi zake zimewekwa katika filamu. Kitaaluma, Hamisi ana shahada ya sanaa (BA Education) ya Chuo Kikuu cha Dares Salaam. Pia, aliwahi kuwa mhariri msanifu wa magazeti ya HabariLEO, Kulikoni, Nipashe pamoja na TBC Digital.
Reviews
There are no reviews yet.