Riwaya ya Kiswahili iliyoandikwa na Hamisi Hussein Kibari, iliyoshinda Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu. Akiwa hana kitu zaidi ya kalamu yake, mwandishi wa habari Walari Saire anaamua kupambana na mfumo kandamizi uliojaa rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka, na wizi wa rasilimali za nchi. Hatua hii inamweka katika hatari kubwa ya kupoteza maisha yake na ya familia yake. Hatimaye anafungwa kwa kubambikwa kesi. Pamoja na madhila anayopitia, huku watu wake wa karibu wakimwonya na kumtaka aache kufuatilia mambo ya wakubwa, Walari anaamua kutorudi nyuma. Lakini makubwa yanampata; anaanza kupoteza watu wake wa karibu sana. Ni yeye sasa, aamue kusuka ama kunyoa. Hamisi Hussein Kibari ni mtunzi wa riwaya na mashairi, mwandishi wa habari, mhariri, na mtengeneza filamu. Kwa karibu miaka 20 ameandika hadithi katika magazeti mbalimbali ya Tanzania na baadhi ya hadithi zake zimewekwa katika filamu. Ana shahada ya BA Education ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Gereza la Kifo
Author(s): classic, Hamisi Hussein Kibari, Kiswahili, mwandishi wa habari, riwaya, rushwa, Tuzo ya Mwalimu Nyerere, Walari Saire
Sh 12,000
Riwaya ya Kiswahili ya Hamisi Hussein Kibari, mshindi wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu. Mwandishi wa habari Walari Saire anapambana na rushwa na ufisadi kwa kalamu yake tu, akiwekwa katika hatari ya kifo. Mwandishi pia ni mtengeneza filamu na mhariri wa magazeti.
ISBN: 9789987417872
Category: Fiction
Tags: classic, Hamisi Hussein Kibari, Kiswahili, mwandishi wa habari, riwaya, rushwa, Tuzo ya Mwalimu Nyerere, Walari Saire
| Dimensions | 195 × 130 mm |
|---|---|
| Binding |
Be the first to review “Gereza la Kifo”Cancel Reply
You may also like…
Related products
-

Divine Providence
Sh 8,000 -

A Wreath for Fr. Mayer
Sh 8,000 -

Mungu Hakopeshwi
Sh 20,000 -

Love Bombs
Sh 15,000

Reviews
There are no reviews yet.