Mkuki Na Nyota Publishers

Edward Moringe Sokoine: Maisha Na Uongozi Wake [Hardback Preorder – shipping from Dec 2024]

(4 customer reviews)

Original price was: Sh 75,000.Current price is: Sh 70,000.

By UONGOZI Institute and Sokoine University of Agriculture (SUA). Available for preorder. Confirmed orders will start shipping in December 2024.

Ni majira ya alasiri, kiasi cha saa tisa hivi, siku ya Alhamisi, Aprili 12, 1984. Ghafla Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD – sasa TBC), redio ya taifa na pekee Tanzania Bara wakati ule, inakatisha matangazo ya vipindi vyake vya kawaida, na Wimbo wa Taifa, Mungu Ibariki Tanzania, unapigwa. Wimbo unamalizika, na sauti iliyozoeleka sana kwa wananchi, lakini zamu hi ikiwa na tulivu mkubwa, inaanza kuelezea taratibu, polepole, tena kwa kituo na majonzi makubwa, ikisema: “Ndugu wananchi, leo mnamo saa saba mchana, ndugu yetu na kijana wetu, Edward Moringe Sokoine, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alipokuwa anarudi Dar es Salaam kutoka Dodoma, gari yake ilipata ajali. Amefariki dunia.” Ghafla, siku iliyokuwa ya kawaida kabisa, watu wakiendelea na Maisha yao na kazi zao na matani yao, ukiwamo utani wa kandanda wa Simba na Yanga, ikawa siku ya msiba mkubwa. Kitabu hiki kinakusafirisha hadi kwenye eneo la ajali iliyokatisha uhai wa kiongozi huyu shupavu, na kinatoa maelezo ya mashuhuda wa ajali hiyo na hata uvumi uliosambaa baada ya kifo chake. Kwa upana wake, kitabu hiki kitakufahamisha maisha halisi ya Hayati Edward Moringe Sokoine, Waziri Mkuu wa tatu wa Tanzania; alikotokea, familia yake na uongozi wake.

Dimensions 150 × 130 mm

4 reviews for Edward Moringe Sokoine: Maisha Na Uongozi Wake [Hardback Preorder – shipping from Dec 2024]

  1. Hon. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    “Natamani kila mtu apate nakala ya kitabu hiki na apate muda wa kukisoma. Kitabu hiki kinachangia, kinaboresha na kinanogesha kwa namna ya pekee kabisa historia ya nchi.”

  2. Joseph Sokoine, Mtoto wa Hayati Edward Sokoine

    “Majaribio mengi ya nyuma ya kuandika kitabu hiki yalishindikana kwa sababu mbalimbali. Katika hali hiyo, ni vigumu kwetu kama familia kupata maneno fasaha ya kuelezea furaha yetu ya kutoka mioyoni kwamba ombi letu hatimaye limeanikiwa na kitabu kuhusu maisha na uongozi wa Mzee wetu kimeandikwa.

  3. Issa Shivji, Profesa-Stahiki wa Sheria na Mchambuzi wa Siasa

    “Viongozi kama Sokoine ambao wanaona mbali na wanajitolea asilimia mia moja kutumikia na kustawisha jamii zao hutokea kwa nadra katika jamii. Katika historia yetu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Edward Moringe Sokoine walikuwa viongozi wa aina hii.”

  4. Donasian Mbonea

    Ndugu Edward Moringe Sokoine alikuwa kiongozi wa pekee, alipiga sana vita kuhusu suala la RUSHWA na uhujumu uchumi, alikuwa Kiongozi mwadilifu na Mzalendo kwa Nchi yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia alitetea HAKI za wanyonge, na alisisitiza sana suala la Kilimo na Nchi kujitegemea kiuchumi bila kutegemea misaada kutoka Ng’ambo.

Add a review

Your email address will not be published. Required fields are marked *