Riwaya ya Kiswahili iliyoandikwa na Philipo Oyaro, mshindi wa Tuzo ya Fasihi ya Kiswahili ya Safal-Cornell mwaka 2023. Aneth, kiongozi wa kampuni ya madini, anakumbwa na masahibu yanayofuatana. Baada ya kubakwa na mtu wake wa karibu kibiashara, anajikuta kizimbani akikabiliwa na mashtaka mazito ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha. Hana kumbukumbu ya kuyatenda hayo, lakini ushahidi unamsulubisha hadharani. Hayo yakiwa bado hayajapoa, ajali ya moto, ikihusisha basi la magereza na lori la mafuta, inaua watu wengi. Aneth pia anadhaniwa kuwa amepoteza maisha, lakini uchunguzi wa polisi unagundua kuwa Aneth si miongoni mwa waliohofiwa kufa. Sakata linachukua sura mpya na kuwaleta pamoja waendesha mashtaka wawili, Dkt. Rehema Nsabi na Zeph Steven, mahasimu wa muda mrefu. Mmoja kati yao ana siri nzito moyoni, siri inayoyatesa maisha yake kwa zaidi ya robo karne. Philipo Oyaro alizaliwa Bunda; ni mwalimu na mwandishi, kwa sasa Mkuu wa Shule ya Mwasa Hope mkoani Mwanza.

Dunia Duara
Author(s): Aneth, Bunda, Kiswahili, madini, Mwasa Hope, Philipo Oyaro, riwaya, Safal-Cornell 2023
Sh 15,000
Riwaya ya Kiswahili ya Philipo Oyaro, mshindi wa Tuzo ya Safal-Cornell 2023. Aneth, kiongozi wa kampuni ya madini, anabakwa kisha kushtakiwa kwa uhujumu uchumi. Ajali ya moto inadhaniwa kumuua, lakini polisi wanagundua kwamba bado yuko hai. Mwandishi ni Mkuu wa Shule ya Mwasa Hope, Mwanza.
| Dimensions | 195 × 130 mm |
|---|---|
| Binding |
You may also like…
-

The African Epic Controversy
Sh 45,000




Reviews
There are no reviews yet.