Mkuki Na Nyota Publishers

Dola, Masoko na Kushindwa kwa Taasisi: Mafunzo Yanayotokana na Kuzaliwa kwa Uchungu Ulioshinikizwa, Maisha ya Mateso, na Kifo cha Maumivu cha MV Bukoba

Authors: Prof. Rwekaza Mukandala

Sh 18,000

Prof. Rwekaza Mukandala

Katika mhadhara huu wa kutafakarisha ujulikanao kwa jina la Dola, Masoko, na Kushindwa kwa Taasisi: Mafunzo Yanayotokana na Kuzaliwa kwa uchungu Ulioshinikizwa, Maisha ya Mateso, na Kifo cha Maumivu cha MV Bukoba, Profesa Rwekaza Mukandala anatumia mkabala wa kihistoria unaoangalia eneo zaidi ya moja, yaani fizikia, sayansi ya siasa, biolojia ya baharini, sheria, na uchumi, kuchunguza sababu kuu zilizochangia kuzaliwa kwa msaada wa kitabibu, maisha ya kuhangaika na yasiyo na furaha, na kifo cha kuumiza kisichotarajiwa.

Dola na masoko vinatazamwa kama “pleti za kitektonik” za jamii zinazochochea matendo ya binadamu. Mhadhara huu unachambua kitunduizi uhusiano baina ya ushiriki wa dola, nguvu za soko, na mifumo dhaifu ya kitaasisi kuonesha namna ambavyo hali mbaya ya kuichumi iliyokuwa ikiikabili Tanzania, uhitaji mkubwa wa chombo cha kutoa huduma za usafiri katika Ziwa Viktoria kufuatia kuanguka kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mifumo dhaifu ya utawala, na kukosekana kwa uwajibikaji kulivyopelekea kutiwa saini kwa mkataba mbovu na wa kunyonya damu, na ununuzi wa chombo kibovu. Mchanganyiko wa taratibu duni za soko, usimamizi mbovu wa sekta ya umma, na mifumo dhaifu va kitaasisi ulisababisha maisha ya mateso ya chombo hicho yaliyohusisha usimamizi duni, kutokujali, uzingatiaii duni wa matatizo ya kistahimilivu yaliyobainika, na taratibu za kiusalama zilizosababisha kifo chake mnamo mwezi Mei mwaka 1996 ambapo chombo husika kilipinduka na kuzama, na kusababisha vifo vva mamia va watu.

Mhadhara huu unasisitiza jinsi udhaifu wa mifumo ya utawala na ukosefu wa uwajibikaji unayvoweza kusababisha maafa makubwa. Profesa Mukandala anapendekeza marekebisho ya taasisi, hasa kupitia Katiba va Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili kuimarisha uwazi, uwajibikaji na maendeleo endelevu katika sekta ya umma na binafsi. Pia, mhadhara huu unakumbusha ghaharama kubwa ya uhai inayosababishwa na kushindwa kwa muda mrefu kuchukua hatua stahiki, na umuhimu wa mageuzi makubwa ya kitaasisi.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Dola, Masoko na Kushindwa kwa Taasisi: Mafunzo Yanayotokana na Kuzaliwa kwa Uchungu Ulioshinikizwa, Maisha ya Mateso, na Kifo cha Maumivu cha MV Bukoba”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…