“Ni wakati tulipokuwa mafunzoni Monduli Machi, 1976 hadi Januari, 1977 ndipo nilipomfahamu vizuri Yusufu Rajabu Makamba na tukawa marafiki tangu wakati huo mpaka sasa. Nikatokea kuutambua vizuri uwezo wake wa uongozi. Nilivibaini vipaji vyake adimu vya kuhamasisha, kuunganisha watu, kujieleza na ubunifu. Pia moyo wake wa kujituma, kutokata tamaa na uhodari wa kazi. Ndiyo maana nilipokuwa Rais nilimteua kuwa Mkuu wa Mkoa na Mbunge na nilipokuwa Mwenyekiti wa CCM nilimteua kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi.”
—Dkt. Jakaya M. Kikwete, Rais wa Awamu ya Nne wa Tanzania
Kuhusu Mwandishi:
Mwandishi wa kitabu hiki, Yussuf Rajabu Makamba, ni mkulima na mfugaji. Amewahi kuwa Mbunge, Katibu Mkuu wa CCM, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, na ni Afisa Mstaafu wa JWTZ. Amewahi pia kuwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kigoma na Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa.
Mwandishi ameandika vitabu vingi ikiwemo ‘Methali, Semi na Vitendawili vya Kisambaa’.
Reviews
There are no reviews yet.