Kuna siri ambazo huzikwa chini ya ardhi. Na kuna nyingine zinazoishi katikati ya watu, zikivaa suti, tabasamu na heshima kubwa mbele ya jamii. Katika jiji la mafanikio ya kiuchumi, ushawishi wa kisiasa na kijamii, na maisha yenye mvuto, kuna nyumba ambayo usiku wake una sauti tofauti. Sauti zinazofifia gizani. Milango inayofungwa kabla ya watu kuuliza maswali mengi. Walinzi wanaolinda zaidi ya ukuta na vivuli vinavyopita kimya kana kwamba vinafahamu jambo ambalo wengine hawapaswi kulijua.
Kila siri ina mwisho wake. Pazia linapoanza kufunguka, kinachoonekana sio ukatili, bali ulimwengu uliojengwa juu ya hofu, tamaa na nguvu zinazolindwa kwa gharama yoyote. Tembea nami kwenye simulizii kujua yaliyojiri.
KUHUSU MWANDISHI
Mayasa Abdallah Chembea, ni mjasiriamali anayeishi jijini Tanga. Ni mwandishi chipukizi na hii ni riwaya yake ya kwanza kuandika na imeshika nafasi ya Kwanza katika Tuzo ya Fasihi ya Safal mwaka 2025.





Reviews
There are no reviews yet.