“Tusiogope” ni tawasifu ya mwanamke jasiri aliteamini kuwa anaweza kufikia malengo yake, na aliyeona fursa pale wengine walipoona changamoto tu. Alijua kuzitumi vizuri fursa hizo, siyo kwa manufaa yake binafsi tu, bali kwa kuwatunuku wengine maarifa, ujuzi na amara ya fedha kwa kadiri ya uwezo wake.
Katika kumbukumbu zake hizi, Bi.Asia Kasuwi Kapande anaelezea kwa uwazi maisha yake ya shule, familia, ajira, kushiriki kwake katika kuanzisha Shirika la Uchumi wa Nyumbani Tanzania na katika siasa; nafasi za usimamizi katika vyuo mbalimbali wa kilimo nchini, na shughuli za kiuchumi na kijamii baada ya kustaafu.
Alikuwa na bahati ya kupata elimu ya juu ndani na nje ya nchi, lakini licha ya hivyo haikuwa kawaida kwa msichana kuajiriwa katika sekta ya kilimo kutokana na mazingira na vikwazo vijana wa kike walivyowekewa. Hakusita. Alikazana kutafuta marifa, na hayo ameyapata nafasi kubwa katika kitabu hiki. Anaeleza jinsi alivyomudu kazi zake kwa kutatua changamoto mbalimbali katika kilimo na ufugaji; mchango wake kwenye masuala ya kukuza elimu, sisa, kusaidia watoto wasiojiweza na wanajamii kwa ujumla kwa kadiri ya uwezo wake.









Reviews
There are no reviews yet.