Miaka minne tu baada ya shambulizi la kigaidi kwenye ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam, mlipuko mwingine wa kutisha unatikisa jiji, safari hii, kwenye ubalozi wa Sweden. Kachero mbobezi, Malik Kweli, anapewa jukumu la kufichua waliohusika, akipokea agizo moja kwa moja kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani. Akishirikiana na msaidizi wake wa karibu, Mohd, wanakimbizana na wakati, wakifanya kazi usiku na mchana kuamua iwapo shambulizi hilo ni sehemu ya njama kubwa ya kigaidi au lina uhusiano mwingine wa kutiliwa shaka. Wanafichua fununu kuhusu wageni wawili wa ajabu waliokuwa jijini kwa miezi miwili na kuondoka siku ya shambulizi. Wakati huo huo, jina la kijana wa mjini, J4, linazidi kutajwa, likizua maswali mapya. Lakini sakata linachukua sura mpya, kiwango kikubwa cha fedha kinatoweka kutoka kwenye tawi la Standard Chartered, moja ya majengo yaliyoathirika na mlipuko.
Je, shambulizi hili lilikuwa kweli kitendo cha ugaidi, au ilikuwa njama ya kihalifu iliyopangwa kwa ustadi wa hali ya juu? Malik na Mohd wanakabiliwa na fumbo hilo, na wanahitaji kulitatua kabla wahusika hawajapotea kabisa.

Dimensions | 195 × 130 mm |
---|---|
Binding |
You may also like…
-
The African Writers’ Handbook
Sh 45,000 -
Ebrahim Hussein
Sh 10,000 -
The African Epic Controversy
Sh 45,000
Reviews
There are no reviews yet.