Riwaya ya Kiswahili ya Anna Samwel Manyanza. Ugumba unaweza kuwa sumu kwenye ndoa. Wasila yamemkuta, kapewa talaka na mumewe Maulidi kwa vile hatungi mimba. Maulidi akaoa upya, tena zaidi ya mara mbili, lakini hakuna katika hawa wakeze aliyeweza kutunga mimba. Huba la Maulidi kwa Wasila likachipua upya; akamtaka Wasila arudi kwa udi na uvumba, kwa mikuki na mapanga. Lakini Wasila alishapelekwa Unguja kwa shangaziye na mjombawe ili walimwengu wasimuandame kwa macho yao ya paka na ndimi zao za swila. Unguja ikamkutanisha Wasila na Bilali. Ugumba wa Wasila ukachukua taswira nyingine. Tumbo la Wasila likaanza kutuna; ni mimba au ni uchuro? Wasila na Bilali wakajikuta wanaelea kwenye bahari ya matumaini iliyo na wimbi la kuzamisha. Moyo wa Bilali ukachukua taswira pacha. Riwaya ya pili ya Anna Samwel Manyanza, mshindi wa Tuzo ya Mabati-Cornell (riwaya yake ya kwanza, Penzi la Damu, Row 329).

Faradhi Ya Moyo
Author(s): Anna Samuel Manyanza, Bilali, Kiswahili, ndoa, riwaya, ugumba, Unguja, Wasila
Sh 18,000
Riwaya ya pili ya Kiswahili ya Anna Samwel Manyanza, mwandishi wa Penzi la Damu (Row 329). Wasila, aliyeachwa kwa ugumba, anapelekwa Unguja na kukutana na Bilali. Tumbo lake linaanza kutuna, lakini ni mimba au uchuro? Hadithi ya ndoa, upweke, na taswira pacha za matumaini.
| Weight | 0.6 kg |
|---|




Reviews
There are no reviews yet.