Mkuki Na Nyota Publishers

Kiguu Na Njia

Sh 15,000

Ben Mtobwa

SKU: 9789987083831 Category: Tag:

Akiwa bado kijana mdogo, Mtukwao anatoroshwa kijijini na familia yake ili aokoe uhai wake ulio katika hatihati ya kupotelea mikononi mwa wanakijiji. Safari inamjia ghafla kama jinamizi na kumfungulia dunia mpya yenye chungu na tamu lakini chungu ni zaidi. Ni pale anapokumbuka kitu muhimu sana alichokipoteza wakati wa pilika zake za maisha, ndipo anapopata wazo la kurudi kwao ili akatengeneze mambo yake. Lakini imekwishapita miaka zaidi ya thelathini tangu aondoke kijijini. Je, familia yake ambayo ndiyo ina dhamana pekee ya kumsaidia, bado ipo? Ama ndiyo ng’ombe wa maskini hazai?

Katika kitabu chake hiki cha mwisho, Ben R Mtobwa anathibitisha kwa mara nyingine uwezo wake mkubwa wa kuitumia kalamu yake bila kubahatisha. Kinachotofautisha riwaya hii na riwaya nyingine za Ben Mtobwa, ni namna mwandishi huyo alivyohama kabisa kutoka kwenye maudhui ya kijasusi na kuchambua uhalisia wa watanzania wengi. Kutana na mhusika aliyetembea karibu kila mkoa, akionesha ama kwa maneno ama kwa matendo, uchumi, jiografia, historia pamoja na mila na desturi za eneo husika.

Weight 0.7 kg

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Kiguu Na Njia”

Your email address will not be published. Required fields are marked *