Mkuki Na Nyota Publishers

Uwazi na Ukweli – 3

Author(s): Awamu ya Tatu, Benjamin W. Mkapa, demokrasia, hotuba, Kiswahili, Millenium Development Goals, MKURABITA, Uwazi na Ukweli

Sh 7,000

Kitabu cha tatu katika mfululizo wa Uwazi na Ukweli cha hotuba za Rais Benjamin W. Mkapa. Inashughulikia utandawazi, demokrasia, usalama wa chakula, Malengo ya Maendeleo ya Milenia, tathmini ya ubinafsishaji, na MKURABITA (Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge).

Kitabu cha tatu katika mfululizo wa Uwazi na Ukweli vyenye mkusanyo wa hotuba za kila mwisho wa mwezi za Mheshimiwa Rais Benjamin W. Mkapa. Sambamba na kuendeleza falsafa yake ya Uwazi na Ukweli, Rais Mkapa anaeleza na kufafanua kwa mapana masuala yanayogusa maslahi ya taifa: utandawazi na ushirikiano baina ya mataifa duniani; demokrasia na wajibu wa viongozi wa mataifa kwa wananchi wao; usalama wa chakula na matatizo ya misaada kutoka mataifa makubwa; maendeleo na ufikiwaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia; na tathmini ya ubinafsishaji. Pia anaeleza Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) ambao Rais anaamini utafungua njia kwa makabwela kujipatia mikopo na mitaji ya kuanzishia na kuendeshea miradi midogomidogo ya kujikimu kimaisha. Kwa Watanzania wote wanaotaka kufuatilia utendaji wa serikali waliyoiweka madarakani.

Weight 0.4 kg
Dimensions 210 × 145 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Uwazi na Ukweli – 3”

Your email address will not be published. Required fields are marked *