Nukuu za Mwalimu Julius K.Nyerere
Julius Kambarage Nyerere alikuwa Rais wa kwanza wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwanzilishi wa taifa hili. Aliingia madarakani kwa kura, uchaguzi wa kidemokrasia uliofanyika mwaka 1961, na alibaki madarakani kwa zaidi ya miongo miwili. Mwalimu Nyerere alikuwa mtu mwenye kipawa na maadili. Alikuwa shujaa wa Afrika, mzalendo, aliyekuwa na kipaji cha kuzungumza, mwenye fikra imara, mwanadiplomasia na juu ya yote, mwalimu. Alichangua kuitwa ‘mwalimu’.
Akiwa madarakani, alitoa mamia ya hotuba; baadhi ziliandaliwa na nyingine bila kuandaliwa. Taasisi ya Mwalimu Nyerere (aliyoianzisha Mwalimu Nyerere mwenyewe, mwaka 1996) imekusanya hotuba na maandiko yake kwenye vitabu.
Nukuu zilizomo katika kitabu hiki, ni zile tu zilizomo katika mfululizo wa vitabu vya Uhuru na mihadhara yake ya chuo kikuu. Zimepangwa katika dhamira zifuatazo; Falsafa, Azimio, Vijiji vya Ushirika, Kujitegemea, Umoja na Mshikamano, Ujamaa, Siasa za ndani, Siasa za Nje, Demokrasia, Elimu, Uongozi, Serikali, Bunge, Ulinzi na Usalama, Jamii na Uchumi.
Reviews
There are no reviews yet.