Huu ni mchezo wa kumi na tisa katika mfululizo wa vitabu vya michezo ya kuigiza kutoka Tanzania Publishing House. Michezo hii, imeendelea kuburudisha na kuelimisha wasomaji wa rika zote tangu ilipochapishwa kwa mara ya kwanza. Kitabu hiki kama vingine katika mfululizo huu, kimechaguliwa kufundishia lugha na drama mashuleni. Kilio Chetu ni tamthiliya inayovunja ukimya uliotawala miongoni mwa jamii katika kutatua matatizo makubwa ambayo chimbuko lake ni mahusiano ya kijinsia.
Katika tamthiliya hii, vijana wanatoa sauti ya jitimai iliyojaa sononeko na shutuma dhidi ya wazazi, walezi na viongozi ambao wanafumbia macho suala hili nyeti. Ndiyo maana tamthiliya hii inasisitiza sana haja ya kuwapa vijana elimu juu ya mahusiano ya kijinsia badala ya hofu na vitisho ambavyo vimedhihirika kupitia hali halisi kuwa vimeshindwa.
Reviews
There are no reviews yet.