Mkuki Na Nyota Publishers

Siku ya Kiswahili

Mkuki na Nyota tukisherehekea Siku ya Kiswahili duniani pamoja na wanafasihi ya kiswahili pale @af_dar ambao ni wadau wetu katika sherehe yetu ya kila mwezi ya #KalamSalaam

Tuliandaa mjadala kuhusu ‘Athari za lugha ya Kiswahili kwenye Fasihi’ ambapo tulijifunza kutoka jopo la wanafasihi nguli kutoka nyanja mbalimbali za kifasihi kama HipHop, Ushairi, Uchapishaji na Uandishi wa Riwaya.

Tungependa kuchukua fursa hii kuwashukuru wajumbe wa jopo @hituwa, @datdudekb, @neema_maria, @williammkufya pamoja na @HellenBulugu ambaye alitoa burudani nzuri kwenye jukwaa letu.

Vilevile tunawashukuru wasanii wote waliotumia fursa ya jukwaa la wazi (Open Mic) kuonesha vipaji vyao. Wasanii mbalimbali wakongwe na chipukizi walitoa burudani ya pekee. Asanteni sana kwa kushiriki!”

HERI YA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI.

Read the full instagram post here.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *