“Kama nisingekuwa na budi kuchagua kitabu kilichoniletea mabadiliko makubwa, basi ningesema ‘Ukombozi wa Wanyama’ cha Peter Singer.”
— Jane Goodall
“Muundo wa uwasilishaji ujumbe wa Singer si wa kimazoea na haufungwi na hisia; ujengaji wake wa hoja ni makini na wenye fikra nzito, kwani hajengi hoja zake kwenye kanuni binafsi wala za kidini wala falsafa ya hali ya juu ya kufikirika, bali katika misimamo ya kimaadili ambayo wengi wetu tayari tunaikubali.”
— New York Times Book Review
“Ni kitabu muhimu sana ambacho kitabadili namna wengi wetu tunavyowachukulia wanyama—na, hatimaye, sisi wenyewe.”
— Chicago Tribune
“Kitabu hiki ni cha lazima…si kwa wapenda wanyama tu bali kwa kila msomaji aliyestaarabika.”
— Cleveland Amory
Tangu chapisho la kwanza kabisa la mwaka 1975, kazi hii yenye kuleta mageuzi makubwa imewaamsha mamilioni ya watu katika kung’amua uwepo wa “uspishi”—kutokujali kwetu kwa kimfumo dhidi ya wanyama wasio binadamu—na hivyo kuchochea harakati kote ulimwenguni za kuleta mabadiliko katika mitazamo yetu kuhusu wanyama na kukomesha kabisa ukatili tunaowatendea.
Katika Ukombozi wa Wanyama, mwandishi Peter Singer anaanika uhalisia wa kutisha wa “mashamba-viwanda ya kisasa” tuliyonayo na hatua za upimaji bidhaa—akitungua hoja muflisi za utetezi, na kupendekeza mbadala wa kile ambacho kimekuja kuwa suala zito la kimazingira na kijamii na vilevile la kimaadili. Huu ni wito muhimu na unaofikirisha kwa dhamiri, usawa, ustaarabu, na haki na ni andiko la msingi lenye kushawishi kwa waunga mkono na hata kwa watia shaka.
Reviews
There are no reviews yet.