Mkuki Na Nyota Publishers

Nimeweza

Authors: Queen Mwanshinga Mlozi

Queen Mwanshinga Mlozi

Mwalimu Queen Mwanshinga Mlozi ana tajiriba pana katika nyunga za elimu na siasa. Katika unga wa elimu, alianza kuwa mwalimu wa daraja la IIIc baada ya hapo, alipanda daraja na kuwa mwalimu wa daraja la IIIA, stashahada, hadi shahada. Amekuwa mwalimu, mwalimu mkuu, mkufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro, na Afisa Elimu wa Manispaa ya Morogoro.
Unga wa siasa, ameshika wadhifa wa ukuu wa wilaya katika Wilaya za Ukerewe, Singida, Urambo na Tabora. Pia, amekuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa wa Wilaya za Singida na Tabora. Hatimaye, aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). Aidha, alikuwa ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC).
Historia ya maisha yake kuzaliwa hadi kustaafu utumishi wa umma, inatuonesha kuwa Mwalimu Queen amepita milima na mabonde.Wakati msomaji anavuka milima na mabonde katika kuitalii safari ya maisha ya Mwalimu Queen, ndipo anambaini Mwalimu Queen kama:mwanamke, mama, kiongozi, na mwanasiasa.
Kutokana na yote hayo, ameipa tawasifu hii jina la “NIMEWEZA”. Miongoni mwa maswali yanayoweza kumjia msomaji ni: “Je ameweza?” “Ameweza nini?” na “Amewezaje?” Majibu ya maswali haya na mengine mengi yamo katika kurasa mbalimbali za tawasifu hii.

Binding

Pages

Year published

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Nimeweza”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…