“Wewe ndiye Christopher Liundi, unayetaka kumchumbia Rahma Simba?”
“Ndiyo mzee, tumependana.” Nikaulizwa tena, “Unajua kuwa Rahma ni Mwislamu? Hivyo hatutaki, hatutaki, hatutaki mtoto wetu aolewe na kafiri?”
Nikamjibu, “Mimi sio dini, namuoa mtu, hivyo kila mmoja wetu ataendelea na dini yake.”
“Ukitaka kuendelea na kazi, achana na Rahma.”
Kuhusu Mwandishi
Balozi Liundi ana shahada (MA) ua Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia ya Siasa ya Uchumi na Uandishi wa Habari kutoka London School of Journalism. Ameshika nyadhifa kadhaa katika chama na serikali, ikiwa ni pamoja na kuwa Katibu Mkuu wa Vijana (TYL), Mkuu wa Wilaya (1978-80), na Balozi wa Tanzania katika nchi za Ufaransa, Ureno, Hispania, Algeria, Ethiopia, Djibouti, Eritrea, na Yemen. Pia, alikuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika mashirika kama UNESCO, WTO, OAU, na ECA kati ya 1993 na 1996. Kati ya 1998 na 20023 alikuwa Mwakilishi wa UNESCO nchini Rwanda na ameshiriki katika juhudi za upatanishi nchini Darfur, Sudan kati ya 20023 na 2005 akiwa pamoja na Dkt. Salim Ahmed Salim.








Reviews
There are no reviews yet.