Kitabu hiki ni mkusanyiko wa barua zilizoandikwa kila wiki, zikizungumza na Azimio (la Arusha) kama mtu aliye hai, anayesikia, anayeulizwa maswali, anayekumbukwa, na wakati mwingine, anakosolewa na anamkosoa mlezi wake, Mwalimu Nyerere. Kupitia barua hizi, tunatembea kutoka enzi za ujamaa, misukosuko ya kiuchumi, mageuzi ya soko huria, mpaka pale Azimio la Arusha linapozikwa na nchi inapokosa mwelekeo. Lakini Azimio hasahauliki. Wananchi wanatamani afufuke, aoteshe mbegu za matumaini mapya.
Kitabu hiki pia kina mazungumzo ya kufikirika, na tafakuri nzito kuhusu ardhi, ajira ya vijana, rasilimali na maisha ya watu wa kawaida. Ni ukumbusho wa tulipotoka, na ni shule muhimu kwa “wajukuu wa Azimio” waliokuta habari zake bila kushuhudia uwepo wake, na wanaoishi ndani ya matokeo ya kila awamu ya kisiasa iliyounda maisha tuliyonayo leo.
Issa G. Shivji ni Profesa Stahiki wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Amechapisha zaidi ya vitabu ishirini, pamoja na makala nyingi za kitaaluma.
Vitabu vingine vilivyochapishwa na Mkuki na Nyota ni ‘Class Struggles in Tanzania’ (toleo la kumbukumbu miaka 50); ‘Constutional and Legal System in Tanzania’; ‘Pan-Africanism or Pragmatism?’; ‘Accumulation in an African Periphery: A Theoretical Framework’ na ‘Development as Rebellion: A Biography of Julius Nyerere’.





Reviews
There are no reviews yet.