Mkuki Na Nyota Publishers

Hazina Mpya: Hadithi Fupi Kutoka kwa Washindi wa Kwanza

Author(s): Anna Samwel Mayanza, Dotto Rangimoto, Halfani Sudi, Lello Mmasi, Mayasa A. Chembea, Philipo Oyaro, Salum Makamba

Sh 10,000

Kama wewe ni mpenzi wa hadithi fupi, hujazo ea kusoma hadithi za Kiswahili, au una muda mchache wa kusoma lakini unatafuta mahali pazuri pa kuanza kuwasoma baadhi ya waandishi mahiri wa Kiswahili, mkusanyiko huu ni mwaliko wa kuingia katika ulimwengu wa simulizi zenye mvuto, zinazosomeka kwa kikao kimoja lakini athari yake hubaki nawe muda mrefu. Hadithi zote katika mkusanyiko huu ni mpya na hazipatikani mahali pengine popote.

VIONJO KUTOKA KWENYE KILA HADITHI

“Mwali wangu hii ndio Perapera. Hapa kichochoroni na hiyo sura yako iliyojaa ushamba wa jiji, mbona utaishia kubakwa. Haya twende kwangu.”

Unajua nini? Kama nilivyosema kuwa kilichonileta Tanzania ni kutafuta uhuru wa siku arobaini, lakini sasa! Sijapata cha uhuru wala cha nini. Kwani nilijikuta kwenye utumwa mpya. Utumwa wa kujitakia.

“Poa tu, mwenye kutega naye anategwa. Mtego utakapofyatukia hukohuko. Akinasa tu kumbakiza lazima, hata kwa ndumba.” * “Hili ndilo nililobaki nalo,” Mama Rehema aliendelea, sauti yake ikiwa ya maumivu, “Viazi hivi… ni vyote nilivyoweza kupata. Nimevichimba mwenyewe asubuhi hii. Tafadhali, Mwalimu…”

“Lakini kwa umbali ule pamoja na redio tuliyoifungulia kwa sauti ya juu wangesikiaje?” Sadifa alijiuliza maswali mtawalia huku akisahau kuwa kuta nazo zina masikio!

“Shekhe Sudy eeeh! Mimi ngoja niwaache. Namuwahi Mzee Ngoweko hapo kwake. Ila usimwache huyo hadi akupe. Haiwezekani watu wa kawaida tupewe, wewe Shekhe mkubwa mtaani hapa unyimwe.”

“Ni nani huyo mume wangu aliyemteka Lulu na kukupigia simu?” Irene aliuliza kwa sauti iliyoambatana na hofu.

Kijana nguvu zilimuisha akatafuta kiti na kukaa, kwa uchungu alimjibu “Ni kizito mno hiki, gharama yake ni maisha yako.” “Sijafahamu.” Halima aliuliza kwa wasiwasi. “Hata mimi sifahamu.”

“Nimekata shauri kurudi nyumbani kwetu Afrika. Nimeteseka vya kutosha hapa Ulaya. Afrika ni paradiso, sasa ndiyo nimefahamu…”

Weight 0.2 kg
Dimensions 195 × 130 × 8 mm

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Hazina Mpya: Hadithi Fupi Kutoka kwa Washindi wa Kwanza”

Your email address will not be published. Required fields are marked *