Katika “Posa za Maana,” Tune Shaaban Salim anachora taswira inayoibua changamoto kati ya mila za jadi na maendeleo ya kisasa. Hadithi inatiririka kupitia macho ya Hamdani, ambaye Maisha yake yanageuka ghafla inapokuja posa ya Tajiri kutoka ughaibuni, ya kutaka kumwoa dda yake, Muna. Pamoja na posa kuwa tetemeko linalotishia umoja wa kifamilia, inafichua pia mvutano wa kitamaduni wa dhamira ya kupata usalama wa kifedha dhidi ya kuyazingatia kwa uthabiti maadili ya jadi. Riwaya hii inachunguza athari za maamuzi katika mambo yanayoonoesha jinsi shauku za mtu binafsi zinavyogusa mshikamano wa jamii, ikiangazia mwingiliano mgumu wa matarajio ya kisasa na urithi wa kitamaduni. “Hebu niambie Salma, umeanza lini hii shauku ya kutaka Muna aolewe? Wewe si ndiye uliyekuwa ukiwafurusha watu kadhaa waliojaribu kuleta posa za Muna? Leo kimezidi nini?” Maneno haya yasiyo na mzaha yanadhihirisha nyufa za kina katika utamaduni uliojizatiti, yakiweka wazi mzozo unaorindima kati ya tunu za zamani na ndoto za baadaye. Ni sauti ya mapambano ya kifamilia, ambapo utii wa mila unapimwa dhidi ya ndoto za kupata mali na furaha.

Dimensions | 195 × 130 mm |
---|---|
Binding |
You may also like…
-
The African Writers’ Handbook
Sh 45,000 -
Ebrahim Hussein
Sh 10,000 -
The African Epic Controversy
Sh 45,000
Reviews
There are no reviews yet.