Mkuki Na Nyota Publishers

Kolonia Santita

Sh 30,000

Enock Maregesi

Hii ni riwaya ya kusisimua ya kijasusi na madawa ya kulevya inayozungumzia vita kati ya Tume ya Dunia ya Umoja wa Mataifa, ya kudhibiti madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa, ‘World Drugs Enforcement Commission’ (WODEC); na shirika kubwa la madawa ya kulevya la Kolonia Santita (CS-14) la Kolombia na Meksiko.

Inaelezea, kwa kinagaubaga, jitihada za pamoja kati ya Tume ya Dunia, Marekani na Meksiko za kuwasaka na hatimaye kuwatia nguvuni viongozi nduli wa CS-14; na kuzuia shehena (kubwa) ya madawa ya kulevya na malighafi ya nyukilia: kwenda Afrika, Asia, Amerika, Ulaya – na kung’oa mizizi ya shirika la CS-14, lote, katika nchi za Hemisifia ya Magharibi – na duniani kwa jumla.

Ukisoma kitabu hiki utajiuliza, “mwandishi huyu aliwezaje kusuka riwaya inayoufanya moyo kukuenda mbio, hata kukulazimu wakati mwingine kukiweka kitabu kando ili urudishe pumzi! Ukishakianza tu, hutakiacha kabla ya kujua mwisho wa vita hii kali ya kimataifa.

Kuhusu Mwandishi

Enock Maregesi ni gwiji wa uandishi wa riwaya za kijasusi na Kolonia Santita, imeweka kiwango kipya cha juu kitakachowaumiza vichwa waandishi wengine katika kutaka kukifikia.

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Kolonia Santita”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…