Wasifu wa Kiswahili wa Edward Moringe Sokoine, Waziri Mkuu wa tatu wa Tanzania, uliochapishwa kwa ushirikiano kati ya UONGOZI Institute na Sokoine University of Agriculture (SUA). Majira ya alasiri siku ya Alhamisi, Aprili 12, 1984, Redio Tanzania Dar es Salaam ilikatisha matangazo ya vipindi vyake vya kawaida, wimbo wa taifa ukapigwa, na sauti iliyozoeleka ikatangaza: Ndugu wananchi, leo mnamo saa saba mchana, ndugu yetu Edward Moringe Sokoine, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alipokuwa anarudi Dar es Salaam kutoka Dodoma, gari yake ilipata ajali. Amefariki dunia. Ghafla, siku ya kawaida ikageuka siku ya msiba mkubwa. Kitabu kinamsafirisha msomaji hadi kwenye eneo la ajali iliyokatisha uhai wa kiongozi huyu shupavu, kinatoa maelezo ya mashuhuda wa ajali na uvumi uliosambaa baada ya kifo chake, na kinamfahamisha msomaji maisha halisi ya Hayati Sokoine, alikotokea, familia yake, na uongozi wake.

Edward Moringe Sokoine: Maisha na Uongozi Wake
Author(s): 12 Aprili 1984, Edward Moringe Sokoine, Kiswahili, SUA, Tanzania, UONGOZI Institute, wasifu, Waziri Mkuu
Sh 75,000
Wasifu wa Kiswahili wa Edward Moringe Sokoine, Waziri Mkuu wa tatu wa Tanzania, aliyefariki kwa ajali ya gari 12 Aprili 1984. Uliandaliwa na UONGOZI Institute pamoja na Sokoine University of Agriculture. Maelezo ya ajali, mashuhuda, uvumi uliosambaa, na maisha ya uongozi wa Sokoine.
| Dimensions | 150 × 130 mm |
|---|




Hon. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania –
“Natamani kila mtu apate nakala ya kitabu hiki na apate muda wa kukisoma. Kitabu hiki kinachangia, kinaboresha na kinanogesha kwa namna ya pekee kabisa historia ya nchi.”
Joseph Sokoine, Mtoto wa Hayati Edward Sokoine –
“Majaribio mengi ya nyuma ya kuandika kitabu hiki yalishindikana kwa sababu mbalimbali. Katika hali hiyo, ni vigumu kwetu kama familia kupata maneno fasaha ya kuelezea furaha yetu ya kutoka mioyoni kwamba ombi letu hatimaye limeanikiwa na kitabu kuhusu maisha na uongozi wa Mzee wetu kimeandikwa.
Issa Shivji, Profesa-Stahiki wa Sheria na Mchambuzi wa Siasa –
“Viongozi kama Sokoine ambao wanaona mbali na wanajitolea asilimia mia moja kutumikia na kustawisha jamii zao hutokea kwa nadra katika jamii. Katika historia yetu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Edward Moringe Sokoine walikuwa viongozi wa aina hii.”
Donasian Mbonea –
Ndugu Edward Moringe Sokoine alikuwa kiongozi wa pekee, alipiga sana vita kuhusu suala la RUSHWA na uhujumu uchumi, alikuwa Kiongozi mwadilifu na Mzalendo kwa Nchi yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia alitetea HAKI za wanyonge, na alisisitiza sana suala la Kilimo na Nchi kujitegemea kiuchumi bila kutegemea misaada kutoka Ng’ambo.