Mkuki Na Nyota Publishers

Moto wa Kifuu

Author(s): Jacob Ngubau Julius

Sh 10,000

ISBN: 9789987086290 Categories: , , , Tag:

Mashairi yaliyomo kwenye diwani hii yanaegemea mkondo wa utunzi wa jadi na lugha yenye uteule na utukufu inayomfanya msomaji kuvutika nayo. Mwandishi ametumia Kiswahili cha kale pamoja na lahaja za pwani ya Kenya kama vile Kiamu, Kimvita, Kitikuu na nyenginezo nyingi. Mbali na lugha ya ufundi yenye ladha ya kutamani kurudiwa enzi na enzi, maudhui yake yanagusa na kuakisi maisha ya kila siku. “Lugha iliyotumiwa ni nzuri mno na imepangwa kwa weledi na mtiririko wa kufurahisha. Kuna mafumbo na nasaha vilevile. Amefaulu kutumia bahari takriban zote za ushairi ikiwemo utenzi.” –Prof. Rocha Chimera

KUHUSU MWANDISHI

Jacob Ngumbau Julius ni mtaalamu wa Habari na Mawasiliano Jijini Nairobi, hata hivyo, njia ya maisha ilimwelekeza katika taaluma ya uhasibu, ambako kwa sasa hutekeleza majukumu yake ya kila siku. Diwani yake ya Moto wa Kifuu ilishika nafasi ya kwanza katika Tuzo ya Kiswahili ya Safal ya Fasihi ya Afrika ya mwaka 2018, wakati huo ikijulikana kama Mabati-Cornell Kiswahili Prize for African Literature. Kando na Moto wa Kifuu, Jacob amekamilisha uandishi wa diwani nyingine ya mashairi, ambayo bado haijachapishwa.

Weight 0.2 kg
Dimensions 195 × 130 × 7 mm

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Moto wa Kifuu”

Your email address will not be published. Required fields are marked *