Riwaya ya kusisimua ya Kiswahili ya Ben Mtobwa kutoka mfululizo wa Joram Kiango. Inspekta Kombora anaitwa katika hoteli moja jijini Dar es Salaam ambapo anaonyeshwa mwili wa msichana aliyeuawa kikatili kupita kiasi. Ngozi na nyama ya uso wake mzima na sehemu ya shingo zimeliwa na aina fulani ya sumu, ikifanya sura yake ibakie kuwa fuvu la kutisha. Katika kinywa cha fuvu hilo uliwekwa ujumbe wa maandishi uliosomeka: Tunamtaka Joram Kiango. Salamu zinamfikia Joram kwa namna nyingine, zikifuatiwa na patashika nzito, watu wengi walio na wasio na hatia wakipoteza roho zao. Lakini ni roho ya Joram Kiango iliyohitajika, kwa udi na uvumba. Naye, akijua kuwa anapambana na mbogo waliojeruhiwa, alichukua tahadhari zote kutopoteza uhai mithili ya paka. Hata roho yake pia inabadilika na kuwa Roho ya Paka.

Roho Ya Paka
Author(s): Ben Mtobwa, classic, Dar es Salaam, Inspekta Kombora, Joram Kiango, Kiswahili, riwaya ya kusisimua, ujasusi
Sh 12,000
Riwaya ya kusisimua ya Kiswahili ya Ben Mtobwa kutoka mfululizo wa Joram Kiango. Mwili wa msichana unapatikana hotelini Dar es Salaam, uso wake umeliwa na sumu na ujumbe mkali unatishia Joram. Inspekta Kombora na Joram wanapambana na adui asiyeonekana, na hatimaye Joram anajifunza kutumia tahadhari ya paka.
| Weight | 0.6 kg |
|---|




Reviews
There are no reviews yet.