Riwaya ya kusisimua ya Kiswahili ya A. E. Musiba kutoka mfululizo wa Willy Gamba. Nyaraka za siri zimeibiwa kutoka ofisi moja ya wapigania uhuru jijini Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania inaingiwa na hofu kuwa nyaraka hizo zitaishia mikononi mwa adui na kuhatarisha maisha ya watu wengi wasio na hatia. Kutokana na ishara maalum, inasadikiwa kuwa majasusi wamekimbilia jijini Nairobi. Mpelelezi nguli Willy Gamba anapewa kazi ya kuwatafuta popote walipo, kwa gharama yoyote, na kuwapokonya nyaraka hizo kabla hawajaziuza kwa adui. Mapambano ya kuwasaka yanazidi kuwa makali, wapelelezi na majasusi wanauwawa, na raia wasio na hatia pia wanaangamia. Willy Gamba anapokutana na mrembo Lina, swali linabaki: yuko upande gani? Na Lulu je? Ni mapambano ya kufa na kupona, na maisha ya wengi yanawategemea.

Kufa na Kupona
Author(s): A. E. Musiba, Dar es Salaam, Kiswahili, mfululizo, Nairobi, riwaya ya kusisimua, ujasusi, Willy Gamba
Sh 8,000
Riwaya ya kusisimua ya Kiswahili ya A. E. Musiba kutoka mfululizo wa Willy Gamba. Nyaraka za siri za Tanzania zimeibiwa, na majasusi wamekimbilia Nairobi. Willy Gamba lazima awapate kwa gharama yoyote kabla hawajaziuza kwa adui. Mapambano ya kufa na kupona yanahusisha warembo wenye siri na adui wasio na huruma.




Reviews
There are no reviews yet.